Mpanda FM

RC Katavi atoa siku 90 kwa DED Mpanda

25 July 2025, 4:50 pm

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akitoa maelekezo. Picha na Samwel Mbugi

“Tengeneza vibanda vijana wafanye biashara katika hadhi”

Na Samwel Mbugi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ametoa agizo la miezi mitatu kwa Mkurugezi wa Manispaa ya Mpanda kuhakikisha vibanda vya stendi kuu Mizengo Pinda vinakuwa katika hali ya usafi ili kuendana na hadhi ya stendi hiyo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wadogowadogo waliopo stendi kuu ambapo amesema ni aibu kuona vibanda vikiwa vimefunikwa kwa mashuka hali inayoonyesha ni uchafu wa mazingira.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa Katavi

Awali akizungumza mkurugezi wa manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli amesema kuwa suala la usafi lipo mikononi mwa kila mmoja katika kuhakikisha takataka zinatolewa kwa wakati pamoja na kuzingatia usafi wa vyoo.

Sauti ya mkurugenzi

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mtandao wa Jamii Forums Afrika uliripoti uwepo vya baadhi ya matundu ya vyoo vilivyoziba jambo lililomuibua Mkuu wa Mkoa kufika katika stendi hiyo na kufanya ukaguzi.