Mpanda FM
Mpanda FM
24 July 2025, 9:47 am

Kimori Chiwa askari muhifadhi kitengo cha utalii hifadhi ya Taifa Katavi. Picha na Anna Mhina
“Tumeweka gharama ndogo ili kila mtanzania aweze kuja kufanya utalii”
Na Anna Mhina
Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kupitia uongozi wa hifadhi ya Taifa Katavi kutoa bei elekezi za utalii katika hifadhi hiyo.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa wanashindwa kuitumia hifadhi yao kwa ajili ya kwenda kujionea vivutio mbalimbali vilivyomo kwa kuhofia gharama ambazo huenda zikawakwamisha.
Kimori Chiwa ni askari muhifadhi kitengo cha utalii hifadhi ya Taifa Katavi amewatoa hofu wanakatavi na kusema kuwa wameweka gharama ndogo ili kila mwanakatavi aweze kunufaika na hifadhi yao.
Katika hatua nyingine Chiwa ameeleza umuhimu wa kutembelea hifadhi ya Taifa Katavi ikiwa ni pamoja na kuona vitu kwa uhalisia na kuongeza uelewa wa kujua baadhi ya vitu.
Hata hivyo hifadhi ya Taifa Katavi ina vivutio mbalimbali kama vile aina tofauti za wanyama, maporomoko ya maji, miti ya matambiko, kumbi za mikutano na chumba cha fungate.