Mpanda FM
Mpanda FM
14 July 2025, 2:16 pm

Afisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Mpanda Irene Samson. Picha na Samwel Mbugi
“Tunashindwa kujikwamua kiuchumi kwa sababu tunapenda starehe”
Na Anna Mhina
Wazazi na walezi mkoani Katavi wametakiwa kusimamia malezi na makuzi ya watoto wao ili kuwaepusha kujiunga na makundi yasiofaa.
Hayo yamesemwa na Irene Samson ambaye ni afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Mpanda kufuatia baadhi ya vijana kushindwa kujikwamua kiuchumi kutokana na kutokuishi uhalisia wao.
Emmanuel Charles, Neema Nelson na Salum Haji ni baadhi ya vijana wa manispaa ya Mpanda wameeleza sababu zinazopelekea kushindwa kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuendekeza starehe na vitu vya anasa.
Hata hivyo mitandao ya Kijamii imekua ikitajwa kama chanzo cha baadhi ya vijana kuishi maisha yasiyo halisi na kusababisha kushindwa kuwajibika kiuchumi.