Mpanda FM

Fursa zasababisha wanaume Katavi kuamka

10 July 2025, 12:53 pm

Mwalimu Chahe (kushoto) akifundisha utengenezaji wa batiki kwa vitendo. Picha na Anna Mhina

“Mafunzo haya walikuwa wanahudhuria kina mama lakini awamu hii wanaume ndio wengi”

Na Anna Mhina

Idadi ya washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali na uchumi imeongezeka hadi kufikia watu 96 kutoka 87 kufuatia ubora wa mafunzo hayo.

Akizungumza baada ya kutamatika kwa mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku tatu meneja wa Mpanda radio FM Denis Mkakala amefurahishwa na idadi kubwa ya wanaume waliojitokeza kwenye mafunzo hayo na kusema kuwa hali hiyo inaashiria matokeo mazuri katika jitihada za kujikwamua kiuchumi kupitia ujasiriamali.

Sauti ya meneja Mpanda radio FM

Mwalimu wa ujasiriamali na uchumi Benjamin Chahe ameushukuru uongozi wa Mpanda radio FM kwa ushirikiano wao katika kuhakikisha wanawapa elimu ya ujasiriamali wananchi wa katavi.

Sauti ya mwalimu Chahe

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza namna mafunzo hayo yatakavyowakwamua kiuchumi.

Sauti ya washiriki

Ikumbukwe kuwa mafunzo hayo ya ujasiriamali na uchumi yaliyoandaliwa na Mpanda radio FM kwa kushirikiana na chuo cha Mkwawa V.T.C kilichopo Iringa mjini yalianza rasmi Julai 7 na kutamatika Julai 9, 2025 katika ukumbi wa CCM wilaya ya Mpanda.