Mpanda FM
Mpanda FM
28 June 2025, 5:17 pm

Mwenyekiti wa CCM Katavi Idd Kimanta. Picha na John Benjamin
“Kiongozi atakaeonesha anamtaka fulani ndani ya chama tutachukua hatua”
Na John Benjamin
Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Katavi kimekemea vikali mianya ya rushwa upangaji wa matokeo kwa wagombea wataojitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi mbali mbali.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Idd Kimanta wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kumekuwa na tabia ya watia nia ngazi ya kata na majimbo kuanza ushawishi wa fedha kwa wapiga kura huku ametoa rai kwa wajumbe na viongozi kujiepusha kuchukua rushwa ambayo inaweza kupelekea kupata wagombea wasio kubarika kwenye jamii.
Katika hatua nyingine Kimanta amekemea vikali kwa baadhi ya wagombea kutoa vitisho kwa wagombea wenzao na kueleza kuwa kila moja anayo nafasi ya kuchukua fomu kugombea kupitia chama hicho na kuwaomba wanawake na vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali kupitia chama hicho.
Chama cha Mapinduzi CCM kimeanza zoezi la ugawaji wa fomu ndani ya chama hicho June 28 kwa watiania katika nafasi za udiwani na ubunge.