Mpanda FM
Mpanda FM
25 June 2025, 8:24 am

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili na afya ya akili Edward Buchee. Picha na Anna Mhina
“Mama mjamzito kama anatumia vilevi anaweza kujifungua mtoto wa aina hiyo”
Na Anna Mhina
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kutoa elimu ya ugonjwa wa ulemavu wa afya ya akili ili kupunguza changamoto hiyo katika jamii.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa hawana uelewa wakutosha kuhusiana na chanzo cha ugonjwa huo.
Edward Buchee ni daktari bingwa wa magonjwa ya akili na afya ya akili katika hospitali ya rufaa Katavi ameeleza baadhi ya sababu zinazopelekea mama kujifungua mtoto mwenye ulemavu wa afya ya akili ikiwemo utumiaji wa vileo wakati wa ujauzito.
Buchee amewasihi wananchi kutowanyanyapaa watoto wenye ulemavu wa afya ya akili kwani kufanya hivyo kunasababisha kuongezeka kwa tatizo.