Mpanda FM
Mpanda FM
20 June 2025, 2:34 pm

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda. Picha na Bertod Chove
“Naiomba jamii tushirikiane kulaani vitendo hivi”
Na Bertod Chove
Diwani Viti maalumu manispaa ya Mpanda Ashura Maganga amelaani vitendo vya wanasiasa wanaofanya ukatili kwa watu wenye ualbino kwa kuamini watashinda katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Ashura ameyasema hayo katika kikao cha kuvunja baraza la madiwani na kuwaeleza wananchi mambo yaliyofanyika ndani ya manispaa ya Mpanda kupitia kata zao ambapo diwani huyo ameiomba kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha wanaweka ulinzi na kuwachukulia hatua watakaobainika kufanya vitendo hivyo.
Kupitia ombi hilo mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph pamoja na katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mpanda wameitaka jamii kulaani vitendo hivyo huku wakidai serikali iko macho kuhakikisha jambo hilo halitokei.
Katika hatua nyingine halmashauri ya manispaa ya mpanda imetumia nafasi hiyo kutambua mchango wa viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya pamoja na madiwani kwa kuwapa vyeti kama ishara ya kutambua utendaji wao wa kazi ndani ya manispaa na mkoa kwa ujumla.