Mpanda FM

Jamii acheni kunyanyapaa watoto wenye ulemavu

19 June 2025, 8:34 am

Picha ya viongozi wa serikali katikati ni mkuu wa wilaya ya Mpanda. Picha na Anna Mhina

“Kumfungia mtoto ndani ni kumnyima haki zake za msingi”

Na Anna Mhina

Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kuondokana na changamoto ya kunyanyapaliwa kwa watoto wenye ulemavu.

Wananchi hao wametoa ombi hilo kufuatia kauli ya mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamil Yusuph ya kuwataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwabagua watoto wenye ulemavu na kuwasababishia kukosa haki zao msingi.

Sauti ya wananchi

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wazazi na walezi kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda

Kupambana na unyanyapaa kwa watoto wenye ulemvu ni wajibu wa jamii nzima na  kuhakikisha watoto hao wanapata upendo na fursa zinazostahili kama watoto wengine.