Mpanda FM

Jamii ielimishwe juu ya umuhimu wa elimu

19 June 2025, 8:19 am

Wanafunzi wakiwa kwenye maandamano siku ya mtoto wa Afrika. Picha na Anna Mhina

“Uelewa mdogo wa jamii juu ya umuhimu wa elimu unatukwamisha tusitimize ndoto zetu”

Na Anna Mhina

Wazazi na walezi mkoani Katavi wametakiwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto ambavyo vinawaathiri kiafya na kisaikolojia.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda alipokuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Jamila Yusuph akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Katavi na kusema kuwa katika kuimarisha ulinzi wa mtoto katika ngazi ya mkoa, wilaya na halmashauri serikali kwa kushirikiana na jeshi la polisi limeanzisha dawati la jinsia la watoto.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amesema wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanatokomeza na kudhibiti ukiukwaji wa haki za watoto.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Tanganyika

Maria Lupunza ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kakoso iliyopo wilaya ya Tanganyika akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya watoto wenzake amebainisha changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo wa jamii juu ya umuhimu wa elimu.

Sauti ya mwanafunzi

Kilele cha maadhimisho ya mtoto wa Afrika kwa mkoa wa Katavi yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mpanda ndogo wilayani Tanganyika yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “HAKI ZA MTOTO TULIPOTOKA TULIPO NA TUENDAKO”.