Mpanda FM
Mpanda FM
12 June 2025, 3:51 pm

Koplo Celsius Mlolele akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi. Picha na Samwel Mbugi
“Unafanyiwa ukatili nyumbani darasani unashindwa kuelewa”
Na Anna Mhina
Wanafunzi mkoani Katavi wametakiwa kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa matukio ya ukatili wa kijinsia ili waweze kutimiza malengo yao.
Hayo yamesemwa na afisa wa dawati la jinsia wanawake na watoto wilaya ya Mpanda afande Veronica na koplo Celsius Mlolele wakati akitoa elimu katika shule ya sekondari Rungwa .
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Rungwa na Mpanda Girls wameipokea kwa furaha elimu hiyo na kueleza namna watakavyotoa taarifa endapo wakiona viashiria vya matendo ya ukatili wa kijinsia.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa shule ya sekondari Rungwa mwalimu Mackson Mapunda amelipongeza dawati la jinsia kwa kufika shuleni hapo na kutoa elimu.
Utoaji wa elimu ya ukatili wa kijinsia katika shule ya sekondari Rungwa ni mpango uliowekwa na Mpanda redio FM katika kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika june 16 mwaka huu.