Mpanda FM
Mpanda FM
2 June 2025, 12:07 pm

Picha ya kitabu cha katiba
“Pia ukisoma katiba utaelewa umuhimu wa kupiga kura”
Na Leah Kamala
Wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni yao kuhusu umuhimu wa kujua na kutambua Katiba ya nchi ili kujenga jamii iliyo na haki, usawa na maendeleo endelevu.
Wakizungumza na Mpanda radio FM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuelewa katiba ya nchi kutawasaidia kujua haki zao.
Sweetbert Nkupilo ni mwanasheria wa kujitegemea amesema kuwa kila mwananchi anapaswa kufahamu maudhui ya msingi ya katiba ili kuhakikisha haki zao zinalindwa pamoja na kuimarisha demokrasia.
Bila kuwa na katiba inayozingatia haki za wananchi, utawala bora, na maendeleo ya taifa jamii inaweza kukumbwa na changamoto ya ukosefu wa haki, Uchumi duni, kudhoofika kwa huduma za kijamii pamoja na matumizi mabaya ya uongozi.