Mpanda FM
Mpanda FM
19 May 2025, 4:22 pm

‘uchafu huo unaotokana na viwanda hivyo zinawasababisha wao kupata mafua ya mara kwa mara na kuharibu biashara zao‘
Na Samwel Mbugi-Katavi
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la jioni linalofanyika eneo la kata ya Mpanda hotel manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamelalamika kuhusu viwanda vya kubangulia karanga vilivyopo katika eneo hilo kusababisha vumbi linaloathiri biashara ya chakula.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Redio FM kuwa uchafu huo unaotokana na viwanda hivyo zinawasababisha wao kupata mafua ya mara kwa mara na kuharibu biashara zao hususani kwa wanaouza chakula.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Ibrahim Msanda amesema kuwa eneo hilo ambalo linatumika kwa wafanyabiashara hao sio eneo la kudumu na utaratibu wa kuwatafutia eneo lingine ambalo litakuwa rafiki unaendelea kufanyika.
Ikumbukwe kuwa mwezi April mwaka huu mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph alimtaka mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli kuhakikisha taka hizo zinazolewa ndani ya siku saba, Hata hivyo jitihada za kumtafuta mkurugenzi zinaendelea ili kutolea ufafanuzi.