Mpanda FM

Wabunge watembelea bandari ya Karema

19 May 2025, 4:05 pm

bandari ya Karema

serikali imejipanga kuifanya bandari ya Karema kuwa kitovu cha biashara

Na betord Chove -Katavi

Wabunge kutoka mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma, ambayo inapakana na Ziwa Tanganyika, Wametembelea bandari ya Karema, kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo pamoja na meli nne kubwa zinazojengwa ili kuimarisha usafirishaji wa mizigo na kukuza biashara.

 Wabunge hao wameonesha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo ambao ni  muhimu katika kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini, hasa katika Ziwa Tanganyika ambalo lina umuhimu kiuchumi na kibiashara kwa Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi na Zambia.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ambaye ameambatana na wabunge hao, ameweka wazi kuwa serikali imejipanga kuifanya bandari ya Karema kuwa kitovu cha biashara, ambapo  Ameeleza kuwa uwekezaji unaoendelea una lengo la kuongeza pato la taifa kupitia biashara ya majini.

Sauti ya Naibu waziri David Kihenzile

Mbunge wa Jimbo la Tanganyika,  Selemani Kakoso, akizungumza na wananchi wa maeneo ya Karema, ametilia mkazo suala la wakandarasi kuzingatia sheria na taratibu za ajira, hususan kuhakikisha wananchi wa maeneo jirani wananufaika kupitia ajira.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Tanganyika