Mpanda FM
Mpanda FM
19 May 2025, 3:30 pm

‘Miche hiyo itasaidia kupunguza ukame na madhara mengine yanayotokana na uharibifu wa mazingira ‘
Na Ban Gadau -Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph Kimaro amegawa miche ya miti zaidi ya laki moja kwa wakazi wa Kijiji cha mbugani kata ya kakese katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa miche hiyo Jamila Yusuph amesema kuwa miti hiyo itasaidia kupunguza ukame na madhara mengine yanayotokana na uharibifu wa mazingira huku akitolea mfano wa tukio la hivi karibuni ambapo nyumba kadhaa ziliezuliwa na upepo mkali kutokana na uchache wa miti ya kutuliza upepo.
Kwa upande wake afisa kutoka Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Oswad Laswai ameendelea kuwahamasisha wananchi kuwa na muamko wa kupanda miti na kuitunza kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Nao baadhi ya wananchi mara baada ya kukabidhiwa miti hiyo wamemshukuru Mkuu wa wilaya kwa jitihada anazo endelea kuzionesha katika kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi kwa kugawa miche hiyo kwa ajili ya ustawi wa kijiji chao na vizazi vijavyo.