Mpanda FM
Mpanda FM
19 May 2025, 2:35 pm

“wataweka wazi mustakabali wao kisiasa na jukwaa gani la kisiasa ambalo wataelekea .“
Na Ben Gadau -Katavi
Wanachama 140 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) Mkoani Katavi wametangaza kukihama chama hicho.
Wakizungumza wanachama hao, wamesema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kutafakari kwa kina kuhusu mustakabali wao kisiasa ndani ya chama hicho.
wamesema siku za hivi karibuni wataweka wazi mustakabali wao kisiasa na jukwaa gani la kisiasa ambalo wataelekea .
Baadhi ya wanachama walioondoka katika chama hicho ni Sifa Gadafi aliyekuwa katibu Bawacha Mkoa wa Katavi,Juma Masoud Kanyere aliyekuwa katibu wilaya ya MLele na Elizabeth Festo katibu BAVICHA Na kaimu katibu BAVICHA mkoa wa Katavi Pamoja na wanachama wengine wa kawaida.