Mpanda FM

Taifa litaathirika vijana msiposhiriki uchaguzi

1 May 2025, 8:18 am

Picha ya Alex Chotora. Picha na Anna Mhina

“Kususia uchaguzi ni kujinyima haki yako”

Na Anna Mhina

Vijana mkoani Katavi wameshauriwa kujitokeza katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ili kuweza kushiriki katika uchaguzi mkuu.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa ngome ya vijana wa chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Katavi Alex Chotora  amesema kuwa kundi la vijana lisiposhiriki katika kutimiza haki ya msingi ya kuchagua viongozi itaathiri taifa kupata viongozi wasio na sifa za kiongozi bora.

Sauti ya mwenyekiti ACT Wazalendo

Kwa upande wake mratibu wa ACT Wazalendo jimbo la Mpanda mjini Erasto Samwel ameeleza namna walivyojipanga katika kutoa elimu ili kuhakikisha wananchi wanashiriki uchaguzi.

Sauti ya mratibu wa ACT Wazalendo

Zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura kwa mkoa wa Katavi linatarajiwa kuanza rasmi may mosi mwaka huu.