Mpanda FM
Mpanda FM
23 April 2025, 2:29 pm

Picha ya Gabriel Elias ni daktari kutoka kituo cha afya cha Town Clinic. Picha na Anna Mhina
“Tupewe elimu ya njia sahihi ya kusafisha sikio”
Na Anna Mhina
Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba Wataalamu wa afya kutoa elimu kusafisha masikio.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wameeleza namna ambavyo wanasafisha masikio yao ikiwemo kutumia vijiti na pamba hali ambayo hupelekea kupata magonjwa ikiwemo kupasuka kwa ngoma ya sikio kutokana na kukosa elimu sahihi ya namna bora ya kusafisha.
Gabriel Elias ni daktari kutoka kituo cha afya cha Town Clinic kilichopo katika halmashauri ya manispaa ya Mpanda ameiasa jamii kuacha kusafisha masikio nyumbani na badala yake wafike kwenye vituo vya afya.