Mpanda FM
Mpanda FM
16 April 2025, 6:56 pm

Picha na Betord Chove
“Tunawapa mafunzo ili waweze kusimamia misimamo inayotekeleza kazi za chama”
Na Betord Chove
Baraza la wanawake la chama cha demokrasia na maendeleo chadema (BAWACHA) Wameanza mafunzo ya uongozi kwa wanachama wanawake mkoani Katavi
Akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo katibu wa Baraza la wanawake Chadema Yusufa Gadafi amesema mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa wanachama ili waweze kutambua wajibu katika kutekeleza mambo mbalimbali yanayohusu chama ikiwemo kampeni ya No reform No election.
Kwa upande wake Rehema Mwacha Mwenyekiti wa Bawacha Kanda ya magharibi na mkufunzi wa mafunzo hayo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa mafunzo ya uongozi ili waweze kusimamia misimamo wanavotekeleza kazi za chama cha demkokrasia na maendeleo.
Kwa upande wao baadhi ya wanawake wanaoshiriki katika mafunzo hayo wameeleza matarajio yao mara baada ya kukamilika kwa semina hiyo elekezi.
Mafunzo hayo yatayofanyika kwa siku mbili yameanza april 16 na yanatarajiwa kukamilika april 17 mkoani hapa Katavi.