Mpanda FM

ACT Wazalendo Katavi yawasihi wanawake kugombea nafasi za uongozi

27 March 2025, 3:55 pm

Picha ya katibu wa ACT Wazalendo Katavi. Picha na Anna Mhina

“Zaidi ya 75% ni nafasi kwa vijana na wanawake”

Na John Benjamin

Chama cha ACT wazalendo Mkoa wa Katavi kimewataka wanawake na vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza katika kipindi cha kumekucha Tanzanzia Gwandu Ndaje katibu wa chama hicho Mkoa wa katavi kuwa na muamko wa kuwania nafasi mbalimbali kuekea uchaguzi mkuu huku akisema zaidi ya asilimia 75 ni nafasi kwa vijana na wanawake kuelekea uchaguzi wa mwezi oktoba.

Sauti ya katibu

Aidha Veronica Kiseo akizungumza kwa niaba ya katibu wa ngome ya wanawake wa chama hicho ameendelea kuwaasa wanawake kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa diwani pamoja na ubunge.

Sauti ya Veronica