

16 March 2025, 3:34 pm
Picha ya Katibu Tawala Wilaya ya Mpanda Jofrey Mwashitete. Picha na John Benjamin
“Serikali inaendelea kuimarisha huduma “
Na John Benjamin
Wananchi wa wilaya ya Mpanda wameishukuru serikali kupitia ofisi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini RITA kwa kuanzisha mfumo wa maombi ya vyeti kwa njia ya kidijitali.
Wananchi hao wamebainisha hayo katika uzinduzi wa kampeni ya elimu ya mfumo wa e-RITA na usajili wa vizazi na vifo ambapo wameleeza kuwa mfumo huo utawasaidia kuwapunguzia gharama za usafri na muda wa kufuatilia vyeti hivyo na wameiomba serikali kuhakikisha wanaendelea kutoa eilimu wananchi wengi zaidi hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Mpanda Jofrey Mwashitete amesema kuwa serikali imeendelea kuwarahisishia wananchi kwa kuendelea kuimarisha huduma zake .
Joseph Njemu ni afisa Rita mkoa wa Katavi amesema kuwa katika wilaya ya Mpanda katika kipindi cha mwaka 2024 hadi 13 march mwaka huu imefanikiwa kusajili vizazi elfu 30 na vifo elfu 10
Kampeni ya utolewaji wa elimu ya mfumo wa e-Rita na usajili wa uzazi na vifo umezinduliwa tarehe 13 mwezi ambapo unatarajiwa kutamatika tarehe 26 ya mwezi mwaka huu.