

16 March 2025, 3:12 pm
Picha ya Dkt Gabriel Elias. Picha na Anna Mhina
“Ni muhimu kuwahi kliniki ili kuepukana na magonjwa hatarishi yanayojitokeza”
Na Edda Enock
Wanawake manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameshauriwa kuwahi kuanza kliniki pale wanapogundua kuwa ni mjamzito ili kupata elimu ya afya ya mama na mtoto.
Ushauri huo umetolewa na Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Town Clinic Dkt Gabriel Elias ambapo amesema kuwa mwanamke anapogundua kuwa ni mjamzito ni muhimu kuwahi kiliniki ili kuepukana na magonjwa hatarishi yanayojitokeza.
Nao baadhi ya wanawake wametoa maoni yao kuhusu umuhimu wa mama mjamzito kuhudhuria mara kwa mara kliniki.
Ili kuhakikisha mama anajifungua salama na mtoto anazaliwa akiwa na afya njema, ni muhimu kuhudhuria kliniki kama inavyoshauriwa na watoa huduma.