

4 March 2025, 2:48 pm
Picha ya Dkt. Gabriel Elias. Picha na Rhoda Elias
“Tupewe elimu juu ya ugonjwa wa apendex”
Na Rhoda Elias
Wananchi wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameomba kupatiwa elimu juu ya ugonjwa wa kidole tumbo (apendex).
Wakizungumza na Mpanda Radio FM wananchi hao wamesema kuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya ugonjwa huo huku wakieleza sababu wanazoelewa.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Town Clinic Dkt. Gabriel Elias ametaja sababu za kitaalam ambazo zinasababisha ugonjwa huo.
Hata hivyo Dkt. Gabriel amesema ugonjwa wa kidole tumbo ni ugonjwa ambao mara baada ya kumpata mtu na kidole tumbo kikishambuliwa, kinaweza kupasuka na kusababisha kifo hivyo jamii izingatie ulaji wa vyakula ambavyo havisababishi maambukizi kwenye tumbo .