Mpanda FM

Wananchi Mpanda watakiwa kutunza vyanzo vya maji

4 March 2025, 2:03 pm

Picha inayoonesha moja ya njia za utunzaji wa vyanzo vya maji. Picha na Leah Kamala

“Wananchi wapande miti kwa wingi ili kulinda vyanzo vya maji”

Na Leah Kamala

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni mseto kuhusiana na umuhimu wa upandaji miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira.

Wakizungumza na Mpanda Radio FM, wananchi hao wamesema kuwa wanapanda miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira na kupata hewa safi.

Sauti ya wananchi

Kwa upande wake Afisa Misitu wa Halmashauri ya Tanganyika Ephraim Luhwago amewasihi wananchi wa mkoa wa Katavi kupanda miti kwa wingi ili kuokoa maisha ya viumbe hai na kulinda vyanzo vya maji.

Sauti ya afisa misitu

Ili kufanikisha juhudi hizo ni muhimu kwa wananchi kutambua faida za kupanda miti ili kusaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii.