

20 February 2025, 4:58 pm
Picha ya mwenyekiti wa shirikisho la umoja wa machinga, Haji Mponda. Picha na Samwel Mbugi.
“Jisajilini ili mkizi vigezo muweze kupata mkopo”
Na Samwel Mbugi
Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo inayotolewa na serikali yenye riba ndogo kupitia umoja wa shirikisho la wa machinga.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa shirikisho hilo Haji Mponda ambapo amewataka wafanyabiashara wadogo wadogo wote kuhakikisha wamejisajili ili kupata vitambulisho ili wakidhidi vigezo vya kupata mkopo huo.
Nae Peter Mwanansila katibu wa shirikisho la la umoja wa wamachinga wilaya ya Mpanda amesema kitambulisho cha machinga kitamsaidia mjasirimali kufanya shughuli zake bila kubugudhiwa na kupata mkopo wenye riba nafuu.
Hata hivyo kuwa fomu kwa ajili ya mkopo huo zinatolewa bila malipo yeyote kwa wajisiriamali wadogo wadogo.