

19 February 2025, 9:15 am
Picha ikionesha takataka zilizotupwa ovyo. Picha na Leah Kamala
“Wananchi watunze mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko”
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameta maoni yao mseto kuhusiana na mandhara ya utupaji holela wa taka katika mazingira.
Wakizungumza na Mpanda radio FM kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema kuwa utupaji holela wa taka husababisha uchafuzi wa mazingira pamoja na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Wananchi wanajukumu kubwa katika kuhakikisha usafi wa mazingira na kupambana na utupaji holela wa taka ili kupunguza changamoto ya magonjwa ya mlipuko.