

13 February 2025, 11:47 am
“Wilaya ya Tanganyika kwa kushirikiana na sekta ya elimu, afya, kilimo na ufugaji wanahakikisha wanasimamia mikakati itakayosaidia kutokomeza hali ya udumavu kwa watoto.”
Na Rachel Ezekekia -Katavi
Wananchi halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wametakiwa kushirikiana na viongozi wa serikali katika mpango wa kutokomeza hali ya udumavu katika wilaya hiyo .
Akizungumza na redio fm mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo buswelu amesema kuwa wilaya ya tanganyika kwa kushirikiana na sekta ya elimu, afya ,kilimo na ufugaji wanahakikisha wanasimamia mikakati itakayosaidia kutokomeza hali ya udumavu kwa watoto.
Aidha amebainisha mipango na mikakati ya wilaya Tanganyika inatekeleza katika kuhakikisha wanaboresha hali ya maendeleo na miradi mbalimbali kwa wananchi katika kipindi cha mwaka huu na miaka ijayo ikiwa ni pamoja na kuboresha hali ya miundombinu kwa usatawi wa wananchi
Katika hatua nyingine ameeleza juhudi za halimashauri ya wilaya ya Tnganyika ambazo zinafanywa kuhakikisha kuna ushirikiano mzuri kati ya wananchi na vyombo vya usalama ili kuhakikisha amani ulinzi pamoja na utulivu unadumishwa katika wilaya ya tanganyika.
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Tanganyika akieleza juhudi zinazofanyika