

10 February 2025, 3:35 pm
Dr. Banuba Deogratias mganga mfawidhi hospitali ya Rufaa mko wa Katavi. Picha na Anna Mhina
“Wananchi wajitokeze kuchunguzwa vimelea vya kifua kikuu”
Wananchi mkoani wa Katavi wametakiwa kujitokeza ili kuchunguzwa vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu Kutokana na uwepo wa mashine mpya za kuchunguza.
Akizungumza na Mpanda Radio FM mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi Banuba Deogratias amesema kutokana na vifaa tiba hivyo mgonjwa anachunguzwa na kuanza tiba mara baada ya kugundulika kuwa na vimelea vya kifua kikuu.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameishukuru serikali kwa hatua hiyo ya kuleta mashine za uchunguzi wa vimelea vya kifua kikuu huku wakiiomba kupatiwa huduma ya vipimo bure kutokana na kuwepo kwa gharama za matibabu.
Haya yamejiri kufuatia hatua ya serikali katika jitihada za kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kwa kugawa mashine mpya 185 zenye thamani ya sh. billion 7 kwa ajili ya uchunguzi na ugunduzi wa vimelea vya ugonjwa huo nchini.