

7 February 2025, 12:18 pm
Picha ya hakimu mkazi mfawidhi Gway Sumaye. Picha na Anna Mhina
“Wananchi watumie mahakama kwa njia ya mtandao ili kuokoa pesa”
Na Lilian Vicent
Wananchi mkoani Katavi wameshauriwa kutumia mahakama kwa njia ya mtandao ili kuokoa muda pamoja fedha zitakazotumika kufutilia madai ya kesi zao.
Akizungumza na Mpanda redio FM hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Katavi Gway Sumaye amebainisha kupitia njia hiyo wameweza kuokoa pesa nyingi.
Sumaye ameongeza kuwa kwa wananchi ambao hawatumii simu janja wanatakiwa kwenda kwenye mahakama za wilaya zilizopo katika maeneo yao kwa ajili kushughulikiwa kesi zao.
Kwa upande wako baadhi ya wananchi wamesema usikilizwaji wa kesi kwa njia ya mtandao utawasaidia watu wanaoishi mbali na mahakama kupata haki zao.
Kwa mujibu wa hakimu mkazi mfawidhi amesema takwimu kwa mwaka 2024 kesi 30 na kuendelea zikihusisha kesi za mahabusu zilisikilizwa kwa njia ya mtandao.