Mpanda FM

Huduma za RITA zawafurahisha wanakatavi

30 January 2025, 12:21 pm

Baadhi ya wananchi wakipatiwa huduma kwenye banda la RITA. Picha na Samwel Mbugi.

“Wananchi wa mkoa wa Katavi wanufaika na zoezi la utoaji wa vyeti vya kuzaliwa”

Na Samwel Mbugi

Baadhi ya wananchi manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamefurahishwa na zoezi la utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ambavyo vinatolewa katika viwanja vya kashaulili ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya sheria.

Wananchi wameyasema hayo wakati wakizungumza na mpanda radio FM kuwa zoezi linaenda vizuri lakini changamoto wanayoiona ni kusubiri kwa muda mrefu baada ya kujisajili.

Sauti ya wananchi

Kwa upande wake afisa habari wa RITA Goodluck Malekela amesema kuwa zoezi hilo linaenda vizuri na mwitikio wa wananchi kujitokeza umekuwa mkubwa kutokana na umhimu wa cheti cha kuzaliwa.

Sauti ya afisa habari wa RITA

Malekela ameeleza changamoto walioibaini kwa baadhi ya wananchi ni uelewa wa kuandika usia ambapo wengi hawana elimu hiyo

Sauti ya afisa habari wa RITA

Hata hivyo zoezi la utoaji wa vyeti vya kuzaliwa katika viwanja vya Kashaulili lilianza rasmi kwenye uzinduzi wa mama Samia Legal AID na litahitimishwa February 2, 2025.