

30 January 2025, 9:40 am
Afisa ustawi wa jamii manispaa ya mpanda mkoani Katavi Anyulumye Longo. Picha na Leah Kamala
“Wazazi watakiwa kushirikiana na walimu kujua maendeleo ya watoto wao”
Na Leah Kamala
Baadhi ya wazazi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema ni wajibu kufuatilia maendeleo ya shule ya watoto wao.
Wakizungumza na Mpanda radio fm, wazazi na walezi wameeleza kuwa wanapaswa kuwa sehemu ya safari ya elimu ya mtoto kwa kushirikiana na walimu.
Afisa ustawi wa jamii manispaa ya mpanda mkoani Katavi Anyulumye Longo amesema kuwa wazazi wana jukumu la kufatilia maendeleo ya mtoto ili kutambua changamoto wanazokumbana nazo wawapo shuleni.
Sauti ya Afisa ustawi wa jamii