Mpanda FM

Wananchi watakiwa kujitokeza kupata elimu ya msaada wa kisheria

24 January 2025, 6:29 pm

Picha ya pamoja ya viongozi wapili kutoka kulia ni mkuu wa mkoa wa Katavi. Picha na Anna Mhina

“Wakurugenzi watakiwa kuhakikisha wanafikisha elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi”

Na Ben Gadau

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha wananchi wanafikiwa na elimu ya msaada wa kisheria  ya mama samia legal aid campaign.

Mrindoko ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya mama Samia ( MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN) iliyofanyika katika uwanja wa kashaulili wilaya ya mpanda Mkoani Katavi huku akiwataka wananchi kuacha kuyaficha matukio badala yake watoe taarifa katika mamlaka husika.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko

Kwa upande wake naibu katibu mkuu wa wizara  ya katiba na sheria Franklin  Rwezumula  amesema  kampeni hii inalenga kupatikana  kwa haki kwa wananchi na kuwataka wananchi kujitokeza kupata huduma hiyo.

Sauti ya naibu katibu mkuu wa wizara  ya katiba na sheria Franklin  Rwezumula 

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama samia ( MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN) wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutambua changamoto zao hivyo kupitia kampeni hiyo zitakwenda kutatuliwa.

Sauti ya wananchi