Kampeni ya mama Samia Legal AID kuzinduliwa rasmi kesho
23 January 2025, 2:30 pm
Picha ya mkuu wa mkoa wa Katavi. Picha na Samwel Mbugi
“Wananchi watakiwa kujitokeza kupata elimu ya msaada wa kisheria”
Na Samweli Mbugi
Wananchi Wametakiwa kujitokeza kupata elimu ya msaada wa kisheria kupitia kampeni ya mama Samia Legal AID inayolenga kutatua changamoto za kisheria ambazo zinawakumba wananchi.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hozza Mrindoko ambapo amesema kampeni hiyo itafanyika kwa siku 10 baada ya kuzinduliwa January 24,2025
Aidha Mrindoko ameongeza kuwa kampeni hiyo itafanyika katika halmashauri zote za mkoa wa Katavi ambapo wananchi waliopo katika Kata 45 na vijiji 114 wataendelea kunufaika na elimu ya msaada wa kisheria
Uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika katika viwanja vya shule ya msingi kashaulili iliyopo manispaa ya Mpanda, na kauli mbiu ya kampeni hiyo ni msaada wa sheria kwa haki usawa amani.