Wanachadema watakiwa kuwa watulivu
21 January 2025, 12:39 pm
Picha na mtandao
“Wanachadema washauriwa kuwa watulivu ili kukamilisha zoezi la uchaguzi”
Na Rhoda Elias – Katavi
Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo [CHADEMA] mkoani Katavi wamesema ni wakati wa chama hicho kumpa nafasi Mgombea Tundu Lissu ili kupata uongozi mpya.
Wakizungumza na Mpanda radio fm wakati wakitoa maoni kuelekea uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika January 21 Wamesema kuwa kwa kipindi kirefu chama hicho kimekuwa chini ya utawala wa Freemani Mbowe hivyo wanatamani chama kimpate mwenyekiti mpya.
Akizungumza kwa njia ya simu mchambuzi wa masuala ya siasa amawataka wafuasi na wanachama wa chama hicho kuwa watulivu na kuepuka migogoro na migawanyiko iliyoanza kujitokeza ili kuweza kukamilisha zoezi la uchaguzi na kumpata kiongozi sahihi.
Kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika january 21, 2025, mkoani Katavi baadhi ya viongozi wa chama hicho wameonekana kuwa na mgawanyiko huku wengine wakimuunga mkono Tundu lissu na wengine wakimuunga mkono Freeman Mbowe kitu ambacho kimemuibua makamu mwenyekiti wa chama hicho mkoani katavi na kuwataka viongozi hao kuzingatia katiba ya chama hicho.