Wazazi wa Kasimba wachoshwa watoto wao kutembea umbali mrefu kufuata shule
21 January 2025, 12:07 pm
“Wananchi wa mtaa wa Kasimba wadhamiria kununua eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi”
Na Lilian Vicent-Katavi
Wananchi wa Mtaa wa Kasimba Kata ya Ilembo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameadhamilia kuchangia kiasi cha shilingi elfu saba na mia tano kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi.
Hayo yamejiri katika mkutano uliofanyika mtaa huo maeneo ya kilimahewa ambapo wamesema shule hiyo itasaidia watoto kutokutembea umbali mrefu ambapo serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba Benard Elias Nsima amewashukuru wananchi kwa kufikia muafaka wa makubaliano kwani changamoto ya uwepo wa shule ni ya muda wa mrefu.
Mussa Athumani ni mtendaji wa kata ya Ilembo amewashukuru wananchi kupokea mradi wa ujenzi wa shule ambapo amebainisha itakwenda kupunguza changamoto kwa wanafunzi hali iliyokua inawafanya baadhi yao kushindwa kupata haki ya msingi ya elimu.
Mradi huo unajumuisha ujenzi wa madarasa sita kwa ajili ya shule ya msingi itakayokuwa ukombozi kwa watoto wanaotembea umbali zaidi ya kilomita tano.