Miundombinu mibovu Mpanda stendi kero kwa madereva
17 January 2025, 9:23 am
“Changamoto wanayoipata madereva ni uwepo wa mashimo ndani ya stend hiyo hali inayopelekea uharibifu wa magari yao“
Na Samwel Mbugi-Katavi
Madereva wanaofanya shughuli zao katika stand ya zamani manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya stend hiyo inayosababisha uharibu wa magari yao.
Hayo yamejiri kufuatia tangazo lililotolewa la kuwataka kuacha kupakia abiria nje ya stendi hiyo kwani baadhi ya magari yamekuwa yakikiuka utaratibu.
Kwa upande wa mwenyekiti na katibu wa madereva katika stend hiyo wamesema kuwa wameunga mkono tangazo la kupinga kupakia nje ya stendi kwani imekuwa ikipelekea magari kupakia abiria wachache.
Hata hivyo Jofrey Tendesi Mwenyekiti wa stendi ya zamani amesema baada ya madereva wanaopakia ndani ya stendi kushindwa kupata abiria wa kutosha jitihada zinafanyika ili kuanza ukarabati hivi karibuni .
Tendesi amebainisha kuwa kwa mujibu wa faini iliyopangwa na manispaa kwa kushirikiana na uongozi wa stendi hiyo kwa magari madogo itakuwa elfu hamsini na magari makubwa faini laki moja .