wananchi mtaa wa Mpadeco walalamikia kutozolewa takataka kwa wakati
14 January 2025, 9:52 pm
“wamelalamikia kutozolewa taka kwa wakati huku wakiwa na hofu kutokana na uwepo wa mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa mpadeco kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia serikali kutokutoa takataka zilizorundikana katika mitaa yao wakihofia kupatwa na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Redio FM kwa nyakati tofauti na kueleza kuwa tatizo la mrundikano wa taka limekuwa sugu kwani zinachukua muda mrefu na kusababisha harufu mbaya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco Ivo Chambala amesema kuna mikakati inafanyika ya kuziondoa hizo takataka ambazo zimesababishwa na uchache wa magari ya kubeba takataka hizo
Hata hivyo Chambala amesema kulingana na taharuki ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu wameanza kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujikinga na ugonjwa huo .
Ikumbukwe kuwa ugonjwa wa kipindupindu kwa mkoa wa Katavi mara ya kwanza ulibainika katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika.