Mpanda FM

Katavi:wananchi washauriwa kuweka malengo ya mwaka ili kutimiza ndoto zao

9 January 2025, 9:31 am

Ponisian Mtui mwanauchumi

kuweka malengo mwanzoni mwa mwaka  husaidia kuepuka matumizi yasiyoyalazima

Na Lilian Vicent -Katavi

Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi wamesema kuwa kuweka malengo mwanzoni mwa mwaka  ni moja ya sababu inayochangia kufikia mafanikio kwa wakati.

Wakizungumza na Mpanda Redio  FM wamebainisha watu wengi wamekuwa wakiweka malengo mengi na kushindwa kuyakamilisha mpaka  mwishoni mwa mwaka.

Sauti za wananchi wakizungumza

Ponisian Mtui ambaye ni mwanauchumi amesema kuweka malengo mwanzoni mwa mwaka  usaidia kuepuka matumizi yasiyoyalazima iwapo utafanya tathimini juu ya  suala husika.

Sauti ya Ponisian Mtui Mwanauchumi

Sanjari  na hayo Posian amesema taasisi au mtu mmoja mmoja wanatakiwa kuweka malengo ili kubainisha mambo ya msingi  na kuyafanyia utafiti kabla ya kuanza utekelezaji.