Katavi:Mbunge jimbo la Nsimbo akabidhi gari ya wagonjwa Itenka
8 January 2025, 12:24 pm
“Amewataka wauguzi na wananchi kutumia gari hilo kwa kufuata kanuni sheria na miongozo ya serikali”
Na Rachel Ezekia-Katavi
Mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Lupembe amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Itenka Kilichopo hlmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Akikabidhi gari hilo la wagonjwa Anna Lupembe Amewataka wauguzi na wananchi kutumia gari hilo kwa kufuata kanuni sheria na miongozo ya serikali na kusema serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata hiyo ikiwemo kuboresha huduma ya nishati na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami .
Sauti ya mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Lupembe
Kwa upande wake Mbonimpaye Nkoronko Akimuwakilisha Mkuu wa wilaya Jamila Yusuph amewataka wananchi wa kata hiyo kutokiuka matumizi ya gari hilo la wagonjwa huku akisisistiza juu ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu
Sauti ya Mbonimpaye Nkoronko Akimuwakilisha Mkuu wa wilaya Jamila Yusuph
Nao baadhi ya wananchi wakizungumza baada ya makabidhiano hayo wameahidi kulitumia kwa mujibu wa sheria na kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa kipindupindu.
Sauti ya baadhi ya wananchi wakizungumza baada ya makabidhiano hayo