Viongozi wa CHADEMA Katavi wamuunga mkono Lisu
3 January 2025, 10:21 pm
“wao kama viongozi wa CHADEMA watahakikisha wanamuunga mkono Tundu Lissu kwa ajili ya maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla.“
Na Edda Enock-Katavi
Viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Katavi Wamemuunga mkono Tundu Lissu Katika kuwania nafasi ya mgombea uenyekiti wa chadema Taifa .
Harson Elimwema ambae ni mwenyekiti wa wilaya ya Mpanda mjini yenye majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni jimbo ya Nsimbo ,na jimbo la Mpanda mjini amewaomba wanachama kumuunga mkono Tundu Lissu kuwa mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Sauti ya Harson Elimwema ambae ni mwenyekiti wa wilaya ya Mpanda
Nao baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo wamesema kuwa wao kama viongozi wa CHADEMA watahakikisha wanamuunga mkono Tundu Lissu kwa ajili ya maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla.
Sauti za baadhi ya viongozi wa CHADEMA aliohudhuria
Chama cha Demokrasia na maendeleao CHADEMA wamefanya mkutano wa tamko la wajumbe wa mkutano mkuu taifa kuelekea uchaguzi mkuu wa chadema taifa,uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika January 21 mwaka huu ..