Jeshi la polisi Katavi labainisha mafanikio kwa mwaka 2024
3 January 2025, 9:34 pm
“kipindi cha mwaka 2024, jeshi la polisi mkoa wa Katavi limefanikiwa kudhibiti wizi wa mifugo ambapo watuhumiwa 48, walikamatwa kwa kosa la wizi wa mifugo“
Na Leah Kamala-Katavi
Jeshi la polisi mkoa wa katavi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 8064 kwa kipindi cha mwezi January hadi December 2024 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2023 ambapo jumla ya watuhumiwa 7831 walikamatwa ikiwa ni pungufu ya watuhumiwa 133 sawa na asilimia 1.7
Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa katavi SACP Kaster Ngonyani na kusema kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa na tuhuma za kujihusisha na matukio ya ukatili wa kijinsia ,uvunjaji, wizi, mauaji, utapeli kwa njia ya mtandao, dawa za kulevya, uuzaji wa pombe moshi pamoja na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali, vifo majeruhi na uharibifu wa mali.
Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi Kaster Ngonyani
Aidha kwa kipindi cha mwaka 2024, jeshi la polisi mkoa wa Katavi limefanikiwa kudhibiti wizi wa mifugo ambapo watuhumiwa 48, walikamatwa kwa kosa la wizi wa mifugo,huku watuhumiwa wengine wakikamatwa na nyara za serikali mbalimbali na walifikishwa mahakamani.
Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi Kaster Ngonyani
Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limeomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa wananchi na kuwataka kutambua kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la wote .