Wajasiriamali Mpanda Hotel waomba eneo mbadala la biashara
20 December 2024, 7:16 pm
“wameiomba serikali ya manispaa ya Mpanda kuwatafutia eneo mbadala la kufanyia biashara zao“
Na Betord Chove -Katavi
Baadhi ya wajasiriamali wanaofanya biashara kando kando ya barabara ya Mpanda hotel Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuwatafutia eneo mbadala mara baada ya serikali kusitisha kufanyabiashara katika eneo hilo ili kupisha uendelezaji wa mradi wa barabara.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM wajasiriamali hao wameiomba serikali ya manispaa ya Mpanda kuwatafutia eneo mbadala la kufanyia biashara zao ili kuendelea kujipatika kipato cha kukimu familia zao.
Sauti za wajasiriamali wakiomba kuwatafutia eneo la kufanyia biashara
Kwa upande wake Paul Kahoya Mkuu wa division ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji manispaa ya Mpanda amesema serikali inaendelea na ufumbuzi wa suala hilo huku akiwataka wafanyabiashara hao kuondoka kwa hiari eneo hilo ili kupisha uendelezaji wa mradi wa barabara.
Sauti ya Paul Kahoya Mkuu wa division ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji manispaa ya Mpanda