Zaidi ya vijana 500 Katavi wanufaika na mradi wa Agri–Connect
27 November 2024, 4:07 pm
“Lengo la mradi ilikuwa ni kuhamasisha vijana kuingia katika shughuli za uzalishaji wa mbogamboga na matunda.“
Na Rachel Ezekia-Katavi
Zaidi ya vijana 500 mkoani Katavi wamenufaika na mradi wa Agri –Connect katika kilimo cha uzalishaji wa mazao yatakayosaidia kupunguza udumavu na kuongeza lishe bora kwa kina mama wajawazito.
Hayo yamebainishwa na Frank Kamnyoge mratibu wa mradi wa Agri –Connect mkoa wa Katavi wakati akiwasilisha mipango kazi ya mradi ambapo lengo la mradi ilikuwa ni kuhamasisha vijana kuingia katika shughuli za uzalishaji wa mbogamboga na matunda.
Sauti ya mratibu wa mradi wa Agri –Connect mkoa wa Katavi Frank Kamnyoge
Kwa upande wake Nehemia james katibu tawala Msaidizi mkoa wa Katavi uchumi na uzalishaji katika kikao hicho amewataka maafisa ugani na maafisa lishe kwenye ngazi ya halmashauri kuendeleza na kusimamia na kutekeleza mradi huo na kuwataka vijana kuwa wabunifu ili kuwasaidia katika uzalishaji.
Sauti ya katibu tawala Msaidizi mkoa wa Katavi
Moja ya vijana mnufaika wa mradi wa agri-connect manispaa ya Mpanda amebainisha fursa aliyoipata kupitia mradi huo kuanzia kwenye uzalishaji hadi upelekaji wa mazao katika soko huku akishauri vijana kutumia fursa ya kilimo katika kujikwamua kiuchumi.
Moja ya vijana mnufaika wa mradi wa agri-connect manispaa ya Mpanda
Mradi wa Agri –Connect ulioanza mwaka 2020 na umefika tamati mwaka huu 2024 .