Mpanda FM

Madereva bajaji Katavi kutotumika kuvunja amani wakati wa uchaguzi

25 November 2024, 1:40 pm

picha na mwandishi wetu

wajibu wao  kuhakikisha hawatumiki kipindi hichi cha uchaguzi wa serikali za mitaa  kuvunja amani .

Na Lilian Vicent – Katavi

Madereva bajaji  Kituo cha soko kuu Manispaa ya Mpanda Mkaoni Katavi wamesema  katika kipindi cha kampeni hawatakubali kutumika kuvunja amani.

Hayo  yamejiri katika kikao  cha mrejesho  wa maagizo Katika kikao na mkuu wa   mkoa wa Katavi pamoja na viongozi wa makundi mbalimbali ikiwemo bajaji katika ukumbi wa manispaa  November 13 mwaka huu.

sauti za madereva bajaji

Frank Kalotho  ambaye  mwenyekiti  wa umoja huo wa bajaji amesema ni wajibu wao  kuhakikisha hawatumiki kipindi hichi cha uchaguzi wa serikali za mitaa  kuvunja amani .

Sauti ya mwenyekiti  wa umoja wa bajaji mkoa wa Katavi

Nae  mkuu wa mkoa wa  Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko katika kikao hicho amesema kuwa waendesha vyombo vya usafiri kama bajaji  wanakutana na watu wengi  hivyo wakigundua viashiria vya uvunjifu wa amani watoe taarifa.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa  Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko

Kampeni   za uchaguzi wa serikali  wa mitaa  zimeanza November 20 hadi November 26 ambapo  kauli mbiu ya uchaguzi wa serikali za mitaainasema    ‘ Serikali za mitaa ,sauti ya wananchi   jitokezee kushiriki uchaguzi’.