Mpanda FM

Katavi: watu 6 wapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu

20 November 2024, 5:36 pm

picha na mtandao

Jumla ya wagonjwa 6 wameripotiwa kupoteza maisha wagonjwa 419 tayari wamesharuhusiwa huku wengine 16 wakiwa bado kwenye uwangalizi

Na John Benjamin -Katavi

Watu  441 wameripotiwa kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu katika tarafa ya Karema kata ya Ikola halmashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.

Akiwasilisha taarifa katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa katavi katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela amesema Septemba 13 hadi Novemba 18 jumla ya wagonjwa 6 wameripotiwa kupoteza maisha wagonjwa 419 tayari wamesharuhusiwa huku wengine 16 wakiwa bado kwenye uwangalizi

Sauti ya katavi katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa wa Katavi waliohudhuria katika kikao hicho wameiomba wakala ya maji vijijini Ruwasa kuhakikisha inafikisha huduma ya maji safi katika shule zote za msingi na sekondari ili kupunguza mlipuko wa ugonjwa huo wa kipindupindu.

Sauti ya wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa wa Katavi waliohudhuria katika kikao

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewaagiza wataalamu wa afya ,wakuu wa idara kuweka mikakati na usimamizi wa namna ambavyo ugonjwa wa kipindupindu  utatokomezwa katika mkoa.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko

Katika kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu kambi kwa ajili uratibu wa shughuli za matibabu naufuatiliaji ilifunguliwa mara baada ya kuthibitisha uwepo wa mlipuko kambi hiyo iliyopo tarafa ya karema kata ya ikola imekuwa eneo muhimu la kuhimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu.