Mpanda FM

Wakuu wa idara Tanganyika watakiwa kutatua changamoto

16 November 2024, 6:02 pm

wakuu wa idara waliohuduria kikao hicho .picha na Rachel Ezekia

acheni kukaa ofisini nendeni mkawahudumie wananchi

Na Anna Milanzi -Katavi

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika ameagiza viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo kusimamia ipasavyo nakuwataka maafisa ugani kuwatembelea wakulima katika mashamba yao .

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa idara wa halmashauri hiyo ambapo amewasisitiza viongozi hao kuacha kukaa ofisini na badala yake wawafikie wananchi hususani katika kipindi hiki cha kilimo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizungumza na wakuu wa idara .picha na Rachel Ezekia

Amesema kuwa idara zote zina haja ya kuhakikisha wanafanya kazi kwa wananchi na kuomba fedha pale inapohitajika kwa ajili ya kufanya  marekebisho ya miundombinu waliyoibaini kuwa na tatizo wakiwa site ili wananchi wapate huduma kwa wakati.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizungumza na wakuu wa idara Tanganyika

Amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa watatuliwe changamoto zinazowakabili kwa wakati katika kila eneo.