Mpanda FM

Kivuko chenye thamani ya Tshs milioni 9.8 chakabidhiwa kwa serikali

15 November 2024, 8:20 pm

Mdau wa maendeleo Injinia Ismail aliyekatikati Katika picha akiwa na wananchi wakati wa makabidhiano ya kivuko .picha na Samwel Mbugi

Baada ya kuombwa na wananchi kusaidia kutengeneza kivuko hicho alifuata taratibu zote na kupata kibali TARURA.

Na Samwel Mbugi -Katavi

Mdau wa maendeleo mkoa wa Katavi Injinia Ismail Nassor Ismail amekabidhi kivuko kwa serikali Chenye thamani ya shilingi milioni tisa (9,800,000/-) kilichopo kata ya Nsemlwa manispaa ya mpanda mkoa wa Katavi.

Makabidhiano hayo yamefanyika November 15,2024 mbele ya viongozi wa serikali na chama cha mapinduzi ambapo amesema baada ya kuombwa na wananchi kusaidia kutengeneza kivuko hicho alifuata taratibu zote na kupata kibali TARURA.

Sauti ya mdau wa maendeleo mkoa wa Katavi Injinia Ismail Nassor Ismail

Baadhi ya wananchi waliofika katika makabidhiano ya kivuko wakiwa wamekaa katika kivuko hicho .picha na Samwel Mbugi

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nsemulwa aliyekabidhiwa kivuko hicho kwa niaba ya serikali Bakari Mhamed Kaponda ametoa shukurani kwa mdau wa maendeleo na kusema kuwa aendelee kuwa na moyo wa kujitolea kwani hayo anayo yafanya ni matendo ya huruma ambayo malipo yake yanalipya na mwenyezi mungu.

Sauti ya diwani wa kata ya Nsemulwa Bakari Kaponda

Wananchi waliojitokeza katika makabidhiano hayo wametoa shukrani kwa mdau wa maendeleo kwa kuona umuhimu wa kusaidia ujenzi wa kivuko hicho ambacho kilikuwa ni changamoto namna ya kuvuka kipindi cha mvua.

Wananchi waliojitokeza katika makabidhiano ya daraja

Hata hivyo Injinia Ismail ameongeza kuwa alishawishika sana baada ya kuona kuna changamoto ya Watoto kupoteza Maisha katika kivuko hicho pindi wanapovuka kuelekea shuleni na wakati mwingine kushindwa kuvuka kutokana na wingi wa maji.

mdau wa maendeleo Injinia Ismail akisalimiana na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika makabidhiano hayo