Mpanda FM

Katavi :Bilion 2.9 kulipa fidia wananchi wanaopisha mradi wa miji 28

14 November 2024, 12:12 pm

Baadhi ya Wananchi ambao wametoa maeneo yao na kupisha mradi wa miji 28 .picha na Lilian Vicent

“ametaka fedha hizo zitumike vizuri sio kuleta  migogoro ndani ya familia.”

Na Lilian Vicent-Katavi

Wananchi 568 wanaopisha ujenzi wa mradi wa miji 28 Katika kata ya shanwe na minsukumilo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wanatarajiwa kulipwa kiasi cha shilingi billion 2.9 kama fidia kwa ajili ya kupisha mradi huo.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa  Mwanamvua Hoza  Mrindoko wakati wa mkutano wa hadhara katika mtaa wa Mtemi beda ambapo ametaka fedha hizo zitumike vizuri sio kuleta  migogoro ndani ya familia.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa mkoa wa Katavi   Mwanamvua Hoza  Mrindoko

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko.picha na Lilian Vicent

Nicholaus Mabula mthamini manispaa ya Mpanda amesema zoezi likianza muhusika aliyefanyiwa uthamini ndie anatakiwa kulipwa  hivyo anapaswa kuwa na nyaraka husika.

Sauti ya Nicholaus Mabula mthamini manispaa ya Mpanda

Iddi Kimanta mwenyekiti wa CCM mkoani Katavi amewashukuru wananchi kwa kuwa wavumilivu kipindi chote  hivyo anaamini fidia hizo hazitachukua muda mrefu.

Sauti ya Iddi Kimanta mwenyekiti wa CCM mkoani Katavi

Nao baadhi ya wananchi wameishukuru serikali kwa kuhakikisha wanapata fedha hizo za fidia licha ya usumbufu waliokuwa wanaufanya kwa viongozi .

Sauti ya wananchi wakizungumza

Mchakato wa  uthamini wa maeneo kwa ajili ya fidia ya kupisha mradi wa maji wa miji 28 katika kata ya shanwe na misunkumilo ulianza tangu mwezi wa 9 mwaka 2023.