Katavi:Vijana wahimizwa kupima afya mara kwa mara
8 November 2024, 3:58 pm
picha na mtandao
” vijana wa kiume hawajitokezi katika suala la upimaji afya zao ikilinganishwa na vijana wa kike.”
Na Rhoda Elias -Katavi
Vijana manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuwa na desturi ya kujitokeza ili kupima afya zao mara kwa mara .
Hayo yamesemwa na Bruno Koronel ambae amekaimu nafasi ya mratibu wa kudhibiti ukimwi Manispaa ya Mpanda,amesema kuwa vijana wa kiume hawajitokezi katika suala la upimaji afya zao ikilinganishwa na vijana wa kike.
Akizungumza na Mpanda Radio FM mratibu huyo ametoa wito kwa vijana kuwa wasisubiri kuona dalili za ugonjwa bali wachukue tahadhari ya kupima afya
Sauti ya Bruno Koronel kaimu mratibu wa kudhibiti ukimwi Manispaa ya Mpanda
Nao baadhi ya vijana wa kiume wametoa maoni yao juu ya upimaji wa afya huku wengine wakisema kuwa uoga wa kupokea majibu endapo wakibainika kuathirika unawafanya washindwe kujitokeza kupima afya.
Sauti ya vijana wakitoa maoni yao
ikumbukwe kuwa tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania inaratibu maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo hufanyika kila mwaka mnamo Disemba mosi.