Wanufaika wa TASAF Katavi watia neno juu ya fedha wanazopokea
8 November 2024, 12:17 pm
Picha na mtandao
“Mfuko huu umeanzishwa kwa ajili ya kupunguza umaskini, kuboresha hali ya wananchi na ili mnufaika aweze kujiunga na TASAF kuna vigezo maalum vinavyohitajika“
Na Lear Kamala- Katavi
Wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF manispaa ya mpanda mkoani Katavi wameishukuru serikali kwa kuanzisha mfuko huo kwani umesaidia kupunguza umaskini kwa kutoa msaada wa kifedha na kuboresha maisha ya wananchi.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM, Wananchi hao wamesema kuwa kupitia mfuko huo wa TASAF wameweza kuboreshewa hali yao ya maisha, kupatiwa msaada wa kifedha, na kuanzisha shughuli za kiuchumi ili kujipatia kipato.
Sauti ya wananchi ambao ni wanufaika wa TASAF
Nae afisa ufuatiliaji wa mpango wa TASAF mkoa wa Katavi Castory Alfredy amesema kuwa mfuko huu umeanzishwa kwa ajili ya kupunguza umaskini, kuboresha hali ya wananchi na ili mnufaika aweze kujiunga na TASAF kuna vigezo maalum vinavyohitajika.
TASAF inalenga kutoa msaada kwa kaya maskini na pia kusaidia kuanzisha miradi ya maendeleo ambayo itaboresha miundombinu ya huduma za kijamii katika mkoa wa katavi.