Katavi:Wananchi wilayani Tanganyika watakiwa kutunza miradi inayotekelezwa na serikali
28 October 2024, 8:59 am
Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbalawa .picha na Ben Gadau
“Miradi hiyo inatokana na pesa zilizopatikana katika mradi wa hewa ukaa ambao ni jumla ya bilioni 22 ambapo vijiji 8 vya halmashauri ya wilaya ya Tanganyika vinanufaika na mradi huo.“
Na Ben Gadau -Katavi
Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kushirikiana kutunza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita ili iweze kuwanufaisha
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbalawa wakati wa akizindua mradi wa zahanati ya Kijiji cha kapanga ulioghalimu kiasi cha shilingi milioni 201 zilizotokana na hewa ukaa.
Sauti ya Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbalawa
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema kuwa zahanati hiyo inatokana na pesa zilizopatikana katika mradi wa hewa ukaa ambao ni jumla ya bilioni 22 ambapo vijiji 8 vya halmashauri ya wilaya ya Tanganyika vinanufaika na mradi huo.
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko
Waziri Makame Mbalawa ametembelea na kuweka mawe ya msingi katika mradi wa maji kijiji cha milala,zahanati ya Kapanga na ujenzi wa barabara ya kalumbi kabatini kata ya katuma.